Psalms 18:10-19

10 aAlipanda juu ya kerubi akaruka,
akapaa juu kwa mbawa za upepo.
11 bAlifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika,
hema lake kumzunguka,
mawingu meusi ya mvua ya angani.
12 cKutokana na mwanga wa uwepo wake
mawingu yalisogea,
ikanyesha mvua ya mawe
na umeme wa radi.
13 d Bwana alinguruma kutoka mbinguni,
sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
14 eAliipiga mishale yake na kutawanya adui,
naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.
15 fMabonde ya bahari yalifunuliwa,
na misingi ya dunia ikawa wazi
kwa kukaripia kwako, Ee Bwana,
kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako.

16 gAlinyoosha mkono kutoka juu na kunishika;
alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
17 hAliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi,
kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.
18 iWalinikabili siku ya msiba wangu,
lakini Bwana alikuwa msaada wangu.
19 jAlinileta nje mahali penye nafasi tele,
akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
Copyright information for SwhNEN